Waungwana,
Hodi hodi kijiweni...
Awali nianze kwa kuomba radhi... It has been a VERY long time tangu ni post anything here (sina hata uhakika kama bado kuna mtu hapa kijiweni).
Well... Unajua tena maisha... Nilifanya uamuzi kurudi Bongo (baada ya takribani miaka kibao huko ughaibuni)...Sikufukuzwa ,na wala maisha haya kunishinda huko (niweke wazi kabisaaa.... maana waswahili wataanza vineno) kama huamini uliza uliza! In "eneway" nilijikuta nimekabwa koo vibaya sana katika kujitayarisha... I mean... mtu umeajiriwa, un akazi za watu na hivyo unajitahidi usije ukaharibu mwishon... at the same time unajaribu kujiweka sawa usije ukaangukia "mwanguko wa mende"... tough nut!!!
In "eneway" nipo Bongo!!! Na kama nilivyoweka kwenye blog "dada" Tanzanian Development Connection nimewasili hapa takribani mwezi sasa... najua wenyeji mtauliza... vipi mbona kimya (?) Sasa wazee simnajua kuku mgeni... hata barazani kwenyewe nilikuwa sipajui.... kidogo kidogo, tunaanza kutokeza pua nje kidogo - at least kuliona jua, nakunawa uso (matongo-tongo kibao)
Kuacha hivyo...Bongo kupo... Wiki chache baadaya kutinga hapa, jamaa mmoja alitahadharisha "Ukija hapa inabidi uingie ki-bongo bongo, ikija ki "unene unene" jamaa ni lazima wakulambe kidogo" Yaani kama jamaa alikuwa anatabiri vile... 2 days later, jamaa waliniingiza mjini na ka-razr kangu nilichokuja nako toka "majuu" kakatoweka "katika mazingira ya kutatanisha"!
Kilio both sides: 1. bei ya ka-razr kwa kweli ina "gandamizaga"... kuipata nyingine kazi (na hapo uwe tayari kuuziwa "sample" au a "knock off" 2. Ni zile information nilizokwisha kuzi save...
Yaani nilijikuta najisemea mwenyewe:
Razr - with memory card $300; SIM card - $1
Information ndani ya simu... 'Priceless"
Ndo Bongo hiyo!!!! Yes, kuna mengi ya kujifunza... Lakini it is Home!!! Na kama wanavyosema "East or west, Home is best! IN addition... I think I can see a tiny tiny tiny light at the other end of this tunnel!!!
Hey, any blogger in Dar? ... tufanye tukutane live basi; wageni tunakuja na shida zetu, lakini msitukimbie jamani:)) Michuzi upo mzee?? Nasikia na Jeff yupo hapa
talk to me...
Ned
Peace
ned
Wednesday, July 04, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment