Friday, July 06, 2007

Diaspora return! - Housing Situation

Waungana,
First thing first: Mtu ukishatua... cha kufanya ni kutafuta pa-kujibanza! Soooo nianze na makazi...
Labda niseme tu... situation yangu ilikuwa tofauti kidogo. As a "displaced" person sikuwa nimejitayarisha na ka "jengo" hapa nyumbani. Baada ya kufanikisha maswala ya "ganda" huko US, niligawa visehemu nilivyokuwa navyo kwa brothers & sisters... - unajua tena. Wakati huo mambo yalikuwa "Mimi Bongo ndo basi tena!" And so hata viwanja nilivyokuwa nimetafuta, niligawa kwa mabwana wadogo etc...
With the benefit of a hind site (wenyewe wanasema hindsite is always 20/20)... nataka tu kukubali kuwa... huo kwa kweli haukuwa msimamo wenye faida kwangu. Unajua kuna ujana na ujana... na kila ujana una mambo yake. Kuna baadhi ya vijana wapo very smart in this area... mimi sikuwa mmojawapo... Hata hivyo, bado kuna chance.. I mean, tunajifuna kutokana na makosa - na maadamu bado tunaishi... "one day yes!"
IN 2006 nilikuja kujaribu kuangalia uwezekano wa kujiweka sawa kabla ya kuja kwa kutafuta japo eneo la kuja kujenga baadaye. Tatizo... machale yakanicheza, nika- chicken out, nikidhani wajanja walikuwa wengi na bei za ka"ki-ploti"zilikuwa "si zenyewe".

Well... freebie of the day!!! Ardhi (na hasa hapa Dar) ni deal ile mbaya!!!! na kwamaoni yangu kwako msomaji, kama huna ka-ploti... fanya juu chini ukipate sasa my friend! Kama una-ka-ploti, lakini hujajenga... jaribu kukamilisha sasa- it is as simple as that!

IN anyway... Kufika hapa ikabidi tuanze kutafuta nyumba ya kupanga! Ni kitu kinachojulikana hapa kuwa ili upate nyumba ni lazima utumie "madalali" (agents)

kwa jinsi tulivyopanga, tulikuwa tunataka kupata maeneo ya Mikocheni, sinza, Kijitonyama, Makumbusho, Msasani etc. Tulidhani ni maeneo mazuri (karibu na mjini:) TATIZO... maeneo hayo ni ghali sana. Kwa mtu unayetaka nyumba ya vyumba 3 (of course with a sebule & a small place to pack your "makopo") you should be looking to shed the upward of $1000 a month (payable in advance on an annual basis) na hiyo unaambiwa ni bei ya "mzawa"! second tatizo...katika maeneo hayo you will be quoted prices in US$
Perhaps what has been the most difficult thing is to try and convince a dalali (and a homeowner) the fact that, not all ya wanao "toka mtoni" wanarudi "loaded"///na kwamba atu kama sisi... ni kweli kuwa hatuna $$ nyingi za kutumia. Tatizo ni kuaminika kuwa kweli huna kitu... I mean... wewe umetoka majuu (kwa Bushi)...what do you mean you do not have money?
IN anyway... ngoja niishie hapa....

talk to me!!!

4 comments:

Anonymous said...

Oi, achei teu blog pelo google tá bem interessante gostei desse post. Quando der dá uma passada pelo meu blog, é sobre camisetas personalizadas, mostra passo a passo como criar uma camiseta personalizada bem maneira. Se você quiser linkar meu blog no seu eu ficaria agradecido, até mais e sucesso. (If you speak English can see the version in English of the Camiseta Personalizada. If he will be possible add my blog in your blogroll I thankful, bye friend).

Anonymous said...

Oi, achei teu blog pelo google tá bem interessante gostei desse post. Quando der dá uma passada pelo meu blog, é sobre camisetas personalizadas, mostra passo a passo como criar uma camiseta personalizada bem maneira. Se você quiser linkar meu blog no seu eu ficaria agradecido, até mais e sucesso.(If you speak English can see the version in English of the Camiseta Personalizada.If he will be possible add my blog in your blogroll I thankful, bye friend).

Anonymous said...

Duh,nakumbuka ulituaga lakini nikadhani unatania fulani hivi.Unajua habari kama hii ni mafunzo mazuri sana kwetu sote tulioko nje na huku tukiwa bado tunahesabu dari na kupanga kurudi nyumbani.Sasa uko wapi?Mbona kimya?Nyumba ulipata?

Anonymous said...

Hello. This post is likeable, and your blog is very interesting, congratulations :-). I will add in my blogroll =). If possible gives a last there on my blog, it is about the Câmera Digital, I hope you enjoy. The address is http://camera-fotografica-digital.blogspot.com. A hug.