Wednesday, May 17, 2006

Emile Augustine Muta AFICHULIWA!!!

Hii story nimeinywa nzima nzima toka wabongo Yahoo group- group ya wabongo hapa Columbus Ohio.

..., tulikuwa tunajiuliza huyu jamma ni nani? Soma story chini hapo!

Habari za mapumziko ya mwishoni mwa wiki watanzania wenzangu na hasa wazalendo.
Narejea tena hewani kama nilivyo ahidi hapo awali kuhusu anayejiita mkimbizi toka Tanzania bwana Emile Augustine Muta.
Narejea tena kusema The Kilimanjaro empire imekuwa na mipango ya muda mrefu sana hasa ukizingatia kabila la Watutsi walivyotapakaa Afrika mashariki na ya Kati kama sio Afrika yote.
Ndugu huyu kama wengine walivyokuwa wanajifanya Watanzania kumbe wamekuja katika shamba la bibi, yeye na wazazi wake wote walikuwa katika kambi ya watutsi iliyokuwa huko Nkwenda Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.
Kama mnakumbuka wakati huo wa Mwalimu watu hawa walipewa huduma sawa na watanzania wengine kuanzia elimu hadi matibabu, na hivo ndugu huyu alisoma Tanzania, na kisha alipata kazi serikalini kama wengine wengi tulivyo waona.
alifanya kazi jijini Dar kwa muda mrefu, lakini baadae alihamishiwa Mkoani Tanga ambako yeye kutokana na kukosa uzalendo na kujali maslahi binafsi, aliugomea uhamisho huo na kuamua kutimkia huko Marekani, ambako kuna dada yake na kisingizio cha kwenda kusoma.
Hajawahi kukamatwa na kutiwa ndani hata mara moja, kwa kuwa serikalini ukiondoka bila ruhusa basi kazi imekwisha na ndicho kilichofanyika kwa ndugu huyu.
Akiwa huko Marekani mwanaye alifariki dunia, yeye hakufika katika msiba huo hadi pale mkewe naye alipofariki dunia ndipo jamaa alikuja kwa muda mfupi kuhudhuria japo, alikuta wamekwisha zika.
Baada ya mazishi jamaa alirejea Marekani, ni kweli kwa mtu anaetafutwa hilo lawezekana na asikamatwe?
Hiyo ndiyo historia fupi ya mtu huyu ambae anatafuta maisha kwa kusema uongo na kulipaka matope taifa letu kwa maslahi yake binafsi. Mtu huyu na wengi kama yeye hawana uchungu na nchi yetu, na ndio maana yuko tayari kufanya chochote bila kujali maslahi ya Tanzania na watanzania kwa ujumla. Anadhani hakuna mtu au watu ambao wangepata kuona habari hizi wakati sasa hivi Dunia iko katika ncha za vidole na hakuna siri.
wanapo sema anaelimu nzuri ni ipi hiyo? mimi ninajua wakati anatimkia huko alikuwa na diploma ya sheria ya Mzumbe!
Ni kweli alikuwa anaheshimika na kabila lake kwa kuwa alikuwa anajitahidi kulinda maslahi yao.
Inatia uchungu sana kuona fadhila zetu sasa zimekuwa ni kupigwa mateke. Imefika wakati sasa sisi watanzania wachache wenye upeo wa kuona mbali kukemea hili, na hata kuwaumbua watu kama hawa kwa kuwasiliana na taasisi walizozidanganya ili kusafisha jina la nchi yetu katika medani za kimataifa.
Kwa leo naomba niishie hapo, naomba niwasilishe.
Ziota.

7 comments:

Anonymous said...

Nafutatilia kisa hiki kwa karibu. Ingewezakana huyu bwana akapatikana ili ajieleze au ajibu shutuma ingekuwa safi sana.

Jeff Msangi said...

Nakubaliana kabisa na Ndesanjo,mnaokaa karibu na hapo anaposema yupo Emil hebu mtafuteni mumsikie hadithi yake.

Anonymous said...

Kijiwe mbona kimedoda?

Rama Msangi said...

simulizi lake bilashaka litakuwa muhimu sana kwa mambo mengi, akipatikana na kulitoa simulizi lake nadhani tutashuhudia haya nisemayo

Anonymous said...


buy viagra [url=http://www.buyviagra-usa.com] buy viagra [/url]http://www.buyviagra-usa.com
Buy Ambien online[url=http://www.buy-ambien.info]Ambien [/url]http://www.buy-ambien.info
Ambien [url=http://www.buyambienwithoutprescription.net] Ambien Without Prescription[/url]http://www.buyambienwithoutprescription.net
Levitra[url=http://www.levitrarxpharmacy.com]Levitra[/url]http://www.levitrarxpharmacy.com

Anonymous said...


Buy Viagra Online viagra online http://www.buyviagraonlinepills.com

Anonymous said...

|
|
|