Wednesday, May 10, 2006

Karibu Kijiweni

Karibu sana "Kijiweni"

Nilipokuwa Bongo - ilikuwa si ajabu kunikuta mitaani, tume "ganda" na washikaji! tunashirikiana michapo (stories). Tulikuwa tukikutana "kijiweni".
Ukifika kijiweni, ni stories baada ya story. Nyingine ni ndoto za maisha, mikasa inayotokea mitaani, nyingine za kufurahisha nyingine za kusikitisha... mradi kila kitu kimo. Hakuna ajenda...mtu unatoka nyumbani huna uhakika utakuta story gani huko kijiweni; lakini ilikuwa ku-miss ni pigo kubwa. Wengine wanaweza kuita sehemu kama hii "Ukumbi wa makoroma" au "barazani"... La muhimu...: Unakaribishwa sana kushiriki!

Kama kawaida "A few ground rules" (Masharti machache ya matumizi):

Masharti YOTE ninaweza kuyaweka katika neno moja:HESHIMA

1. Heshima ni kitu cha bure. Tafadhali andika kama unazungumza na mtu aliyesimama mbele yako - na mnajuana kikamilifu.

2.TAFADHALI jaribu kujiweka wazi... kwa kweli hakuna haja kabisa ya kujificha ficha nyuma ya majina kama "Anonymous" - By the way, unajua kuna namna ya kutambua jina la mwandishi (hata kama emejificha kwa kutumia an alias name)? Kutumia "Anonymous" haimaanishi mtu akitaka kukujua hawezi!

3.Maswala yote yanayohusu unyumba, uchi na vitu kama hivyo hayatavumiliwa hapa "kijiweni" Kama unasoma maandishi haya una umri wa kutosha na bila shaka unaelewa kabisa ninachokisema!

4.Kwetu waTz - tunaheshimu "kichwa chenye mvi". Baadhi yetu huwa tunapata "Mshtuko wa moyo" tunapoona watu wanadharau wazee wanaojulikana ni wakubwa kiumri. Kweli tunatumia "keybodi" kuwasiliana... lakini kuna watu wanafahamika kuwa wenye mvi (mfano viongozi wa zamani ambao wamstaafu n.k. Tafadhali tumia busara na kuonyesha heshima.

5.Ni marufuku, kutukana, kuapa, au kuweka maandishi au picha inayojaribu kuonyesha kadamnasi kwamba wewe ndio umekasirika kichizi!

6.Changia au shambulia wazo... sio utu wa mtu!

Masharti haya nafuu ni kwa faida yetu wote.... Uvunjaji wa masharti haya nafuu hautavumiliwa! Na kama mwenyeji wako itabidi tukufungie nje!

Mwenyeji wako
Edmond

1 comment:

Anonymous said...

how does one join this blog