Thursday, May 11, 2006

Wabongo wengine bwana!!!!! - Inabidi tubadilike

Waungwana,

Awali kabisa ni lazima niweke wazi kuwa sina uhakika kama huyu Emil ni mBongo! Sio tu inakuwa ngumu sana kwangu kukubali kuwa waTz tumefikia kiwango cha chini namna hii; bali pia kutokana na ukweli kuwa Emil hakutumia jina lake la mwisho... na hivyo inakuwa ngumu sana kuhakikisha kama yeye ni mTz; au ni mtu wa kuja anajaribu kutumia mgongo wa wengine... Uwezekano huu wa jamaa kutokauwa mBongo ndio unachochea nia yangu ya kuandika kama ninavyoandika hapa (ambapo nitaandika kwa kuassume kuwa jamaa ni mmbongo - kama alivyodai).

Nina amini kabisa kuwa sote (waTz) tuna wajibu wa kumuumbua mtu yeyote anayejaribu kujinufaisha kibinafsi kwa stories za kipuuzi zinazogharimu heshima yetu waTz kama watu waaminifu (ukilinganisha na mataifa mengine tunayoyajua - naogopa kushtakiwa:). Ninachosema ni kuwa kama jamii ni lazima tuwe tayari kuumbua tabia kama hizi! Hata kama mimi mwenyewe ningefanya kama huyu bwana au nitajikuta nimefanya kama huyu ndugu yetu - nitastahili kufanyiwa hivyo hivyo!

Sasa nafahamu kabisa umuhimu wa kuonyesha huruma, na upendo n.k n.k. Nafahamu wengi tuliopo huku ughaibuni... wakati mwingine inabidi mtu uwe "underground" n.k n.k. Lakini ni vizuri kukumbuka kuwa jamii ni jinsi tunavyoitengeneza wenyewe! Ukimya kwa kitu kama hiki sio jibu.

KWa maoni yangu...huyu bwana tapeli period!
Kwake yeye faida yake Binafsi, haina bei! Hata kama ni kuwaibisha waTz milioni 38; kwake yeye heshima na credibility yetu sote kama taifa - kwake yeye ni gharama ndogo sana ukilinganisha na tamaa aliyonayo - Kiurahisi kabisa... inaonyesha jinsi "ubinafsi" ulivyojikita ndani yake! ... What a looser!
Sasa tufanye nini?
La kufanya ni kumtoa hadharani! - Yes, najua baadhi mtaniona "noma" au "kinaa" au ...whatever man! I am just disgusted by his behavior!
Ndesanjo amelalamika kuwa hicho kitu hata hajakisikia... ndugu, ndio utapeli wenyewe huo...hiyo story nifix babu kubwa! Dawa = nikumuibua peupeeee!

Iwapo kila mmoja wetu atatuma email kwa mwandishi (ambaye nadhani ni mchungaji wake) na kwa mhariri wa gazeti la The Lutheran - nadhani watapata ujumbe!
Kuhusu mhariri, tutie shinikizo la kumwomba atumie njia zozote anazozifahamu - ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na KKKT (ELCT - Eveng. Lutheran Church of Tanzania); kupata uhakika wa story ya Emil.
Halafu, sidhani kama itakuwa too much kumtaka aweke story nyingine ya kuwafahamisha wasomaji wake kuwa the whole story of Emil was a shameless, lowly and cheap scam against the people of Tanzania.
Huenda I am taking this too personal! Lakini kama mtanzania - hasa ninayeishi huku ughaibuni... najisikia kama vile mtu kanitukania mzazi wangu!

Kibaya zaidi ni kuwa... kwa story kama hii, hata kama kuna watu walikuwa wana nia ya kweli kabisa kusaidia waTz waliopo huklu ughaibuni - au hata nchi kwa ujumla...sasa inakuwa ngumu kwa sababu ya upuuzi wa mtu mmoja!
In anyway jazba pembeni:
Aliyeandika hiyo article ni Mchg. Charles N. Bailey wa kanisa la Kilutheri "All Saints" Lutheran Church Auburn Kent, Washington; ambaye nina hakika ni mtu mzuri anayejaribu kusaidia waumini wake kwa kila namna anayoweza. Ni kwa vile tu tapeli amempata!
Inawezekana kabisa wewe na mimi ndio tegemeo pekee la hawa wazungu wa watu kuupata ukweli wa mambo! Aidha kwa Mchg. Bailey - hili linaweza kuwa bomu kwake! Hebu fikiria iwapo msharika mmoja atapata taarifa kuwa jamaa tapeli... unadhani itakuwa shida kufikiria kuwa huenda Emil ana njama na Mchg? In anyway, kuwaandikia si kuwatia aibu ni kuweka wazi na kupasua jipu ambalo tusipo fanay hivyo matokeo yanaweza kuwa mabaya zaidi!
Sikuweza kupata email binafsi ya Mchg. Lakini contacts za hilo kanisani ni:
27225 Military Rd S
Auburn, WA 98001-1808
Simu: 253-852-4884
email: aslcauburn@comcast.net
Mtandao: http://www.aslcauburn.com/index.htm

Kuhusu The Lutheran magazine. Email ya mharirini: utheran@thelutheran.org

Ned

3 comments:

John Mwaipopo said...

Hii story nimeisoma pale kwenye gazeti na pengine ni wakati sasa tusipuuze yaliyomo. Ama kuwa upande wake huyu Emil ama upande wa ukweli uliko. Cha msingi tufanye uchunguzi kamili na tujue kilichopi. Kwa mfano tumtafute Kamishna wa Uhamiaji bongo atufafanulie. Si vema kumshambulia tu Emil pasi na kujua ukweli ama uwongo.

Maoni haya ni kwa mtu kama mimi ambaye sielewe chochote kuhusu huyu jamaa. Mnaomfahamu wala msimuonee haya endapo anachafua jina la Bongo.

mloyi said...

Kijiwe cha wabongo. wabongo wote tutajumuika.
Tunategemea mengi toka hapa sisi tunatembeleana sana kama vile tuko wanakokuita uswahilini, usishangae siku utakapopata wageni wengi mpaka uanze kuwafukuza.
Karibu sana.

Jeff Msangi said...

Ned,
Mimi nakuunga mkono kabisa.Nimewapigia hao jamaa na wameniambia wanalifuatilia kwa karibu suala hili.
Mwaipopo,kuna habari zinazostahili uchunguzi zaidi na zisizostahili.Hii nadhani haistahili.Maombi gani ya viza aliyokuwa anayapitisha huyu bwana.Wapinzani gani anawaongelea?Labda mtu aniambie kwamba palikuwa na miscommunication kati ya alichosema Emil na alichoandika mchungaji.Lugha zinaweza kupishana wakati mwingine.