Thursday, November 19, 2009

Still in Bongo

Wow!
IT has been over 2 years... and yes, I am still in Bongo!
You may be wondering... what is the big deal?
Well, let me just say - it is and has been a big deal! Can you try to figure out how many of waTz wanatafakari mchana na usiku on how they can take the leap and return back home? - let me just say... A LOT of them. and thus it is very big deal kuamua na actually kurudi "nyumbani".
Unajua tatizo ni: ukweli kuwa uamuzi huo ni mgumu sana. - Na hasa kama mtu umeweza
kujiweka sawa, una kazi yako nzuri tu, na you have finally figured out on how to do life... katika mazingira kama hayo, a decision to re-locate back to Tz - is a big deal my friend. Na ukweli ni kuwa, one should think of that decision as such!

Kwa upande wangu, mwanzo haukuwa rahisi. Tulitua Dar mwishoni mwa April 2007! By Mid August - binafsi nilikuwa tayari ku-pack and return back to America (where I knew how things work, and could live a life with a certain degree of certainty).
Things were "so hard" that I seriously question my sanity! Now I must qualify with a "hind-site" observation that; the "hardness" was primarily from my expectations /my mindset! Things were not working out as I expected... but my MINDSET made it harder to make anysense of what was going on.
Lets see...BY that time:
1: Tulikuwa hatujui container letu lipo wapi - ingawa tulipata taarifa limefika, na we did not think anything was wrong - until ilipofika wakati wa kwenda kukagua - only to go and find the container is "Nowhere to be seen" - yo can imagine our shock!
2. Vigari vyetu vilikuwa bado vimekwama bandarini... jamaa walikuwa wanadai kodi kama zao!
3. Hatukuwa tumejitayarisha na mahali pa kuishi (kumbuka tulisha hama - "for good"!), na tulikuwa hatupati nyumba ya kupanga iliyo-fit our budget na "description". Kwa sababu ya kuja na a "pre-conceived idea" of where I want to leave and in what way; it become impossible for us to find an ideal house. The fact kuwa every landlord wanted tomake extra cash (in $) coupled by a "whaky" real estate market didn't make things any easier. Kuna wakati ilibidi mimi na watoto wangu tulale katika hostel ya waroma - for 2 weeks!na bado jamaa walikuwa wana charge $35 and $45 per room. THAT WAS so hard to swallow! But it knocked some sense into me! INfact it was during that time that I knew I MUST change my mindset - otherwise WE WILL DIE!
hapo huja weka what we saw ourseleves as consistently struggling with the pace and the way things works (in ALL aspects of life); Wajanja wana ku"lamba" left n' right... i mean.. it was as if jamaa walikuwa wamepania ku "wahi vidola kabla havijaisha" - it was NOT a good experience!

Sasa ni rahisi kuona kuwa The reality of "home coming" was not all that rosy! And at that time it was very tempting to think and actually kudai "this place has no system" and "nothing works!". BUT kama kuna ukweli ni kuwa... THAT IS NOT TRUE...
THERE IS a system here (in Bongo), and YES THINGS WORKS! - it is just that they work very differently from what we knew how things works! Things works here!
Friend, I am convinced knowing this for sure is a deal breaker, if one has to make a successful re-entry! YOUR PERCEPTION on this IS EVERYTHING!

Probably, mtego mkubwa sana ni iwapo mtu uliondoka hapa ukiwa ushakuwa mtu mzima. Mtego wenyewe ni kwamba mtu unakuwa una "memory" of how things works... unakuwa unaelewaa "culture" ya Bongo etc.
Tatizo ni ukweli kuwa "culture" is a very dynamic concept. Culture IS NEVER static; na a mere fact kwamba umeishi katika mazingira tofauti, with a very different system, and a very different world view of things, hiyo tu ina tosha ku change so much of who you are, and how you see things; often without you knowing that you have changed at all. na kwa hiyo mtu unarudi hapa na uelewa wako.. only to find that "that" understanding actually is absolute - and does not work!
NI lazima mtu uwe tayari kukubali ukeli kuwa kuwa; ukirudi hapa, you WILL NOT be coming back the same person.This you must accept and prepare to face the consequence of that reality.

And so... if there is one thing I can say to all who plans to return home ni kwamba:
Think it through, na ikifikia ume amua kurudi nyumbani, YOU MUST also prepare and actually work on your attitude! Vitu hapa haviendi kama tulivyozoea huko ughabuni... and yet that is not synonymous to "things do not work" Ukirudi Bongo na mindset ya "things need to work this way" - utaumia. That is almost a guarantee my friend.

Having said that... niseme tu:
This is probably "THE BEST" decision I have made in my life. I am now used to life here, and to be very honest with you I LOVE IT! I mean really loving it! Of course hii haina maana U.S ndo basi tena.. infact tuna makazi na nyumba huko, inawezekana kabisa kurudi! Lakini pia ni ukweli kuwa east or west, home is best! I am now convinced; the trajectory of my life here is brighter kuliko nilivyokuwa US. Of course challenges hazikosekani - they are everywhere! Lakini kama ni future... inang'aa zaidi hapa kuliko nilivyokuwa U.S. Am I dilusional.. Absolutely NO.
How?... that is topic for another time.

Until then...
ciao my friend.

Ned

Friday, July 06, 2007

Diaspora return! - Housing Situation

Waungana,
First thing first: Mtu ukishatua... cha kufanya ni kutafuta pa-kujibanza! Soooo nianze na makazi...
Labda niseme tu... situation yangu ilikuwa tofauti kidogo. As a "displaced" person sikuwa nimejitayarisha na ka "jengo" hapa nyumbani. Baada ya kufanikisha maswala ya "ganda" huko US, niligawa visehemu nilivyokuwa navyo kwa brothers & sisters... - unajua tena. Wakati huo mambo yalikuwa "Mimi Bongo ndo basi tena!" And so hata viwanja nilivyokuwa nimetafuta, niligawa kwa mabwana wadogo etc...
With the benefit of a hind site (wenyewe wanasema hindsite is always 20/20)... nataka tu kukubali kuwa... huo kwa kweli haukuwa msimamo wenye faida kwangu. Unajua kuna ujana na ujana... na kila ujana una mambo yake. Kuna baadhi ya vijana wapo very smart in this area... mimi sikuwa mmojawapo... Hata hivyo, bado kuna chance.. I mean, tunajifuna kutokana na makosa - na maadamu bado tunaishi... "one day yes!"
IN 2006 nilikuja kujaribu kuangalia uwezekano wa kujiweka sawa kabla ya kuja kwa kutafuta japo eneo la kuja kujenga baadaye. Tatizo... machale yakanicheza, nika- chicken out, nikidhani wajanja walikuwa wengi na bei za ka"ki-ploti"zilikuwa "si zenyewe".

Well... freebie of the day!!! Ardhi (na hasa hapa Dar) ni deal ile mbaya!!!! na kwamaoni yangu kwako msomaji, kama huna ka-ploti... fanya juu chini ukipate sasa my friend! Kama una-ka-ploti, lakini hujajenga... jaribu kukamilisha sasa- it is as simple as that!

IN anyway... Kufika hapa ikabidi tuanze kutafuta nyumba ya kupanga! Ni kitu kinachojulikana hapa kuwa ili upate nyumba ni lazima utumie "madalali" (agents)

kwa jinsi tulivyopanga, tulikuwa tunataka kupata maeneo ya Mikocheni, sinza, Kijitonyama, Makumbusho, Msasani etc. Tulidhani ni maeneo mazuri (karibu na mjini:) TATIZO... maeneo hayo ni ghali sana. Kwa mtu unayetaka nyumba ya vyumba 3 (of course with a sebule & a small place to pack your "makopo") you should be looking to shed the upward of $1000 a month (payable in advance on an annual basis) na hiyo unaambiwa ni bei ya "mzawa"! second tatizo...katika maeneo hayo you will be quoted prices in US$
Perhaps what has been the most difficult thing is to try and convince a dalali (and a homeowner) the fact that, not all ya wanao "toka mtoni" wanarudi "loaded"///na kwamba atu kama sisi... ni kweli kuwa hatuna $$ nyingi za kutumia. Tatizo ni kuaminika kuwa kweli huna kitu... I mean... wewe umetoka majuu (kwa Bushi)...what do you mean you do not have money?
IN anyway... ngoja niishie hapa....

talk to me!!!

Wednesday, July 04, 2007

Hodi Hodi Bongo!!!

Waungwana,
Hodi hodi kijiweni...
Awali nianze kwa kuomba radhi... It has been a VERY long time tangu ni post anything here (sina hata uhakika kama bado kuna mtu hapa kijiweni).
Well... Unajua tena maisha... Nilifanya uamuzi kurudi Bongo (baada ya takribani miaka kibao huko ughaibuni)...Sikufukuzwa ,na wala maisha haya kunishinda huko (niweke wazi kabisaaa.... maana waswahili wataanza vineno) kama huamini uliza uliza! In "eneway" nilijikuta nimekabwa koo vibaya sana katika kujitayarisha... I mean... mtu umeajiriwa, un akazi za watu na hivyo unajitahidi usije ukaharibu mwishon... at the same time unajaribu kujiweka sawa usije ukaangukia "mwanguko wa mende"... tough nut!!!

In "eneway" nipo Bongo!!! Na kama nilivyoweka kwenye blog "dada" Tanzanian Development Connection nimewasili hapa takribani mwezi sasa... najua wenyeji mtauliza... vipi mbona kimya (?) Sasa wazee simnajua kuku mgeni... hata barazani kwenyewe nilikuwa sipajui.... kidogo kidogo, tunaanza kutokeza pua nje kidogo - at least kuliona jua, nakunawa uso (matongo-tongo kibao)
Kuacha hivyo...Bongo kupo... Wiki chache baadaya kutinga hapa, jamaa mmoja alitahadharisha "Ukija hapa inabidi uingie ki-bongo bongo, ikija ki "unene unene" jamaa ni lazima wakulambe kidogo" Yaani kama jamaa alikuwa anatabiri vile... 2 days later, jamaa waliniingiza mjini na ka-razr kangu nilichokuja nako toka "majuu" kakatoweka "katika mazingira ya kutatanisha"!
Kilio both sides: 1. bei ya ka-razr kwa kweli ina "gandamizaga"... kuipata nyingine kazi (na hapo uwe tayari kuuziwa "sample" au a "knock off" 2. Ni zile information nilizokwisha kuzi save...
Yaani nilijikuta najisemea mwenyewe:
Razr - with memory card $300; SIM card - $1
Information ndani ya simu... 'Priceless"

Ndo Bongo hiyo!!!! Yes, kuna mengi ya kujifunza... Lakini it is Home!!! Na kama wanavyosema "East or west, Home is best! IN addition... I think I can see a tiny tiny tiny light at the other end of this tunnel!!!

Hey, any blogger in Dar? ... tufanye tukutane live basi; wageni tunakuja na shida zetu, lakini msitukimbie jamani:)) Michuzi upo mzee?? Nasikia na Jeff yupo hapa

talk to me...
Ned
Peace
ned

Wednesday, May 17, 2006

Emile Augustine Muta AFICHULIWA!!!

Hii story nimeinywa nzima nzima toka wabongo Yahoo group- group ya wabongo hapa Columbus Ohio.

..., tulikuwa tunajiuliza huyu jamma ni nani? Soma story chini hapo!

Habari za mapumziko ya mwishoni mwa wiki watanzania wenzangu na hasa wazalendo.
Narejea tena hewani kama nilivyo ahidi hapo awali kuhusu anayejiita mkimbizi toka Tanzania bwana Emile Augustine Muta.
Narejea tena kusema The Kilimanjaro empire imekuwa na mipango ya muda mrefu sana hasa ukizingatia kabila la Watutsi walivyotapakaa Afrika mashariki na ya Kati kama sio Afrika yote.
Ndugu huyu kama wengine walivyokuwa wanajifanya Watanzania kumbe wamekuja katika shamba la bibi, yeye na wazazi wake wote walikuwa katika kambi ya watutsi iliyokuwa huko Nkwenda Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.
Kama mnakumbuka wakati huo wa Mwalimu watu hawa walipewa huduma sawa na watanzania wengine kuanzia elimu hadi matibabu, na hivo ndugu huyu alisoma Tanzania, na kisha alipata kazi serikalini kama wengine wengi tulivyo waona.
alifanya kazi jijini Dar kwa muda mrefu, lakini baadae alihamishiwa Mkoani Tanga ambako yeye kutokana na kukosa uzalendo na kujali maslahi binafsi, aliugomea uhamisho huo na kuamua kutimkia huko Marekani, ambako kuna dada yake na kisingizio cha kwenda kusoma.
Hajawahi kukamatwa na kutiwa ndani hata mara moja, kwa kuwa serikalini ukiondoka bila ruhusa basi kazi imekwisha na ndicho kilichofanyika kwa ndugu huyu.
Akiwa huko Marekani mwanaye alifariki dunia, yeye hakufika katika msiba huo hadi pale mkewe naye alipofariki dunia ndipo jamaa alikuja kwa muda mfupi kuhudhuria japo, alikuta wamekwisha zika.
Baada ya mazishi jamaa alirejea Marekani, ni kweli kwa mtu anaetafutwa hilo lawezekana na asikamatwe?
Hiyo ndiyo historia fupi ya mtu huyu ambae anatafuta maisha kwa kusema uongo na kulipaka matope taifa letu kwa maslahi yake binafsi. Mtu huyu na wengi kama yeye hawana uchungu na nchi yetu, na ndio maana yuko tayari kufanya chochote bila kujali maslahi ya Tanzania na watanzania kwa ujumla. Anadhani hakuna mtu au watu ambao wangepata kuona habari hizi wakati sasa hivi Dunia iko katika ncha za vidole na hakuna siri.
wanapo sema anaelimu nzuri ni ipi hiyo? mimi ninajua wakati anatimkia huko alikuwa na diploma ya sheria ya Mzumbe!
Ni kweli alikuwa anaheshimika na kabila lake kwa kuwa alikuwa anajitahidi kulinda maslahi yao.
Inatia uchungu sana kuona fadhila zetu sasa zimekuwa ni kupigwa mateke. Imefika wakati sasa sisi watanzania wachache wenye upeo wa kuona mbali kukemea hili, na hata kuwaumbua watu kama hawa kwa kuwasiliana na taasisi walizozidanganya ili kusafisha jina la nchi yetu katika medani za kimataifa.
Kwa leo naomba niishie hapo, naomba niwasilishe.
Ziota.

Thursday, May 11, 2006

Wabongo wengine bwana!!!!! - Inabidi tubadilike

Waungwana,

Awali kabisa ni lazima niweke wazi kuwa sina uhakika kama huyu Emil ni mBongo! Sio tu inakuwa ngumu sana kwangu kukubali kuwa waTz tumefikia kiwango cha chini namna hii; bali pia kutokana na ukweli kuwa Emil hakutumia jina lake la mwisho... na hivyo inakuwa ngumu sana kuhakikisha kama yeye ni mTz; au ni mtu wa kuja anajaribu kutumia mgongo wa wengine... Uwezekano huu wa jamaa kutokauwa mBongo ndio unachochea nia yangu ya kuandika kama ninavyoandika hapa (ambapo nitaandika kwa kuassume kuwa jamaa ni mmbongo - kama alivyodai).

Nina amini kabisa kuwa sote (waTz) tuna wajibu wa kumuumbua mtu yeyote anayejaribu kujinufaisha kibinafsi kwa stories za kipuuzi zinazogharimu heshima yetu waTz kama watu waaminifu (ukilinganisha na mataifa mengine tunayoyajua - naogopa kushtakiwa:). Ninachosema ni kuwa kama jamii ni lazima tuwe tayari kuumbua tabia kama hizi! Hata kama mimi mwenyewe ningefanya kama huyu bwana au nitajikuta nimefanya kama huyu ndugu yetu - nitastahili kufanyiwa hivyo hivyo!

Sasa nafahamu kabisa umuhimu wa kuonyesha huruma, na upendo n.k n.k. Nafahamu wengi tuliopo huku ughaibuni... wakati mwingine inabidi mtu uwe "underground" n.k n.k. Lakini ni vizuri kukumbuka kuwa jamii ni jinsi tunavyoitengeneza wenyewe! Ukimya kwa kitu kama hiki sio jibu.

KWa maoni yangu...huyu bwana tapeli period!
Kwake yeye faida yake Binafsi, haina bei! Hata kama ni kuwaibisha waTz milioni 38; kwake yeye heshima na credibility yetu sote kama taifa - kwake yeye ni gharama ndogo sana ukilinganisha na tamaa aliyonayo - Kiurahisi kabisa... inaonyesha jinsi "ubinafsi" ulivyojikita ndani yake! ... What a looser!
Sasa tufanye nini?
La kufanya ni kumtoa hadharani! - Yes, najua baadhi mtaniona "noma" au "kinaa" au ...whatever man! I am just disgusted by his behavior!
Ndesanjo amelalamika kuwa hicho kitu hata hajakisikia... ndugu, ndio utapeli wenyewe huo...hiyo story nifix babu kubwa! Dawa = nikumuibua peupeeee!

Iwapo kila mmoja wetu atatuma email kwa mwandishi (ambaye nadhani ni mchungaji wake) na kwa mhariri wa gazeti la The Lutheran - nadhani watapata ujumbe!
Kuhusu mhariri, tutie shinikizo la kumwomba atumie njia zozote anazozifahamu - ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na KKKT (ELCT - Eveng. Lutheran Church of Tanzania); kupata uhakika wa story ya Emil.
Halafu, sidhani kama itakuwa too much kumtaka aweke story nyingine ya kuwafahamisha wasomaji wake kuwa the whole story of Emil was a shameless, lowly and cheap scam against the people of Tanzania.
Huenda I am taking this too personal! Lakini kama mtanzania - hasa ninayeishi huku ughaibuni... najisikia kama vile mtu kanitukania mzazi wangu!

Kibaya zaidi ni kuwa... kwa story kama hii, hata kama kuna watu walikuwa wana nia ya kweli kabisa kusaidia waTz waliopo huklu ughaibuni - au hata nchi kwa ujumla...sasa inakuwa ngumu kwa sababu ya upuuzi wa mtu mmoja!
In anyway jazba pembeni:
Aliyeandika hiyo article ni Mchg. Charles N. Bailey wa kanisa la Kilutheri "All Saints" Lutheran Church Auburn Kent, Washington; ambaye nina hakika ni mtu mzuri anayejaribu kusaidia waumini wake kwa kila namna anayoweza. Ni kwa vile tu tapeli amempata!
Inawezekana kabisa wewe na mimi ndio tegemeo pekee la hawa wazungu wa watu kuupata ukweli wa mambo! Aidha kwa Mchg. Bailey - hili linaweza kuwa bomu kwake! Hebu fikiria iwapo msharika mmoja atapata taarifa kuwa jamaa tapeli... unadhani itakuwa shida kufikiria kuwa huenda Emil ana njama na Mchg? In anyway, kuwaandikia si kuwatia aibu ni kuweka wazi na kupasua jipu ambalo tusipo fanay hivyo matokeo yanaweza kuwa mabaya zaidi!
Sikuweza kupata email binafsi ya Mchg. Lakini contacts za hilo kanisani ni:
27225 Military Rd S
Auburn, WA 98001-1808
Simu: 253-852-4884
email: aslcauburn@comcast.net
Mtandao: http://www.aslcauburn.com/index.htm

Kuhusu The Lutheran magazine. Email ya mharirini: utheran@thelutheran.org

Ned

Unakaribishwa kijiweni II

Waungwana,
Ili kutimiza nia ya kuruhusu watu kuweza kutundika "stories" hapa "Kijiweni", Inabidi nikualike rasmi.
Tafadhali jisikie huru kuweka comment yenye anwani yako ya email ili nikutumie ukaribisho.
Ndesanjo & Mwaipopo, nashukuru sana kwa kunitembelea.. karibuni sana wazee
Ned

Wednesday, May 10, 2006

Baadhi yetu Wabongo inabidi tubadilike!

Rafiki yangu mmoja amenitumia hiki kisa cha huyu jamaa "Emil" anayedai kuwa mTz. Kwa ufupi jamaa ni fix tupu! Au sijui niseme ni noma kichizi! Stiry yake ni ya uongo usio na kifani. Ati amekimbia Tz kwa sababu ya fujo za kisiasa - eti kwa sababu alikuwa ameamua kutenda haki kama mkristo safi.
Jamaa kaja Marekani - kawazuga wazungu (kulia, kushoto, kwetu kinyerezi, baba kwame ni mjomba wangu) wazungu wamelewa hata haisimuliki!

Story imeandikwa kwenye gazeti la kilutherani "The Lutheran"

Story inaanza:
"...Meet Emil. Like Job of the Old Testament, he has been tested and blessed by a God of grace and unconditional love.
That our paths should meet at all reflects God’s creative genius—and a divine sense of humor. Imagine a God who weaves together the stories and hearts of a small Lutheran church (of Scandinavian descent) in the Seattle area and the story and heart of Emil, a stranger from Tanzania. Tragedy and redemption, loss and blessing, faith and restoration. That’s Emil’s story—and now it’s ours too.
....Emil Augustine was a well-
educated 36-year-old who held a prestigious position in the Tanzanian government. He had a nice home, two growing boys and a wife who worked as a nurse. He was respected in his tribe and traveled the country using his ability to speak five languages.
Then his life began to unravel.When a new political party took control, he was instructed not to give visas to any of the opposition’s leaders. A Christian, Emil chose to uphold the Tanzanian constitution, which allowed any citizen of good standing to leave the country. After one warning, he was arrested and thrown in jail without trial..."
Waungwana, jisomeeni mwenyewe hapa. Uongo bin nuksi!
Ni nini maoni yako? Kama mtanzania, nini tunaweza kufanya kujikinga na watu kama hawa? By the way huyu jamaa ni mtanzania kweli?
Mawazo yangu ya nini wee na mimi tunaweza kufanya kukomesha hii nuksi = next posting.
Ned

Karibu Kijiweni

Karibu sana "Kijiweni"

Nilipokuwa Bongo - ilikuwa si ajabu kunikuta mitaani, tume "ganda" na washikaji! tunashirikiana michapo (stories). Tulikuwa tukikutana "kijiweni".
Ukifika kijiweni, ni stories baada ya story. Nyingine ni ndoto za maisha, mikasa inayotokea mitaani, nyingine za kufurahisha nyingine za kusikitisha... mradi kila kitu kimo. Hakuna ajenda...mtu unatoka nyumbani huna uhakika utakuta story gani huko kijiweni; lakini ilikuwa ku-miss ni pigo kubwa. Wengine wanaweza kuita sehemu kama hii "Ukumbi wa makoroma" au "barazani"... La muhimu...: Unakaribishwa sana kushiriki!

Kama kawaida "A few ground rules" (Masharti machache ya matumizi):

Masharti YOTE ninaweza kuyaweka katika neno moja:HESHIMA

1. Heshima ni kitu cha bure. Tafadhali andika kama unazungumza na mtu aliyesimama mbele yako - na mnajuana kikamilifu.

2.TAFADHALI jaribu kujiweka wazi... kwa kweli hakuna haja kabisa ya kujificha ficha nyuma ya majina kama "Anonymous" - By the way, unajua kuna namna ya kutambua jina la mwandishi (hata kama emejificha kwa kutumia an alias name)? Kutumia "Anonymous" haimaanishi mtu akitaka kukujua hawezi!

3.Maswala yote yanayohusu unyumba, uchi na vitu kama hivyo hayatavumiliwa hapa "kijiweni" Kama unasoma maandishi haya una umri wa kutosha na bila shaka unaelewa kabisa ninachokisema!

4.Kwetu waTz - tunaheshimu "kichwa chenye mvi". Baadhi yetu huwa tunapata "Mshtuko wa moyo" tunapoona watu wanadharau wazee wanaojulikana ni wakubwa kiumri. Kweli tunatumia "keybodi" kuwasiliana... lakini kuna watu wanafahamika kuwa wenye mvi (mfano viongozi wa zamani ambao wamstaafu n.k. Tafadhali tumia busara na kuonyesha heshima.

5.Ni marufuku, kutukana, kuapa, au kuweka maandishi au picha inayojaribu kuonyesha kadamnasi kwamba wewe ndio umekasirika kichizi!

6.Changia au shambulia wazo... sio utu wa mtu!

Masharti haya nafuu ni kwa faida yetu wote.... Uvunjaji wa masharti haya nafuu hautavumiliwa! Na kama mwenyeji wako itabidi tukufungie nje!

Mwenyeji wako
Edmond