Wednesday, May 10, 2006

Baadhi yetu Wabongo inabidi tubadilike!

Rafiki yangu mmoja amenitumia hiki kisa cha huyu jamaa "Emil" anayedai kuwa mTz. Kwa ufupi jamaa ni fix tupu! Au sijui niseme ni noma kichizi! Stiry yake ni ya uongo usio na kifani. Ati amekimbia Tz kwa sababu ya fujo za kisiasa - eti kwa sababu alikuwa ameamua kutenda haki kama mkristo safi.
Jamaa kaja Marekani - kawazuga wazungu (kulia, kushoto, kwetu kinyerezi, baba kwame ni mjomba wangu) wazungu wamelewa hata haisimuliki!

Story imeandikwa kwenye gazeti la kilutherani "The Lutheran"

Story inaanza:
"...Meet Emil. Like Job of the Old Testament, he has been tested and blessed by a God of grace and unconditional love.
That our paths should meet at all reflects God’s creative genius—and a divine sense of humor. Imagine a God who weaves together the stories and hearts of a small Lutheran church (of Scandinavian descent) in the Seattle area and the story and heart of Emil, a stranger from Tanzania. Tragedy and redemption, loss and blessing, faith and restoration. That’s Emil’s story—and now it’s ours too.
....Emil Augustine was a well-
educated 36-year-old who held a prestigious position in the Tanzanian government. He had a nice home, two growing boys and a wife who worked as a nurse. He was respected in his tribe and traveled the country using his ability to speak five languages.
Then his life began to unravel.When a new political party took control, he was instructed not to give visas to any of the opposition’s leaders. A Christian, Emil chose to uphold the Tanzanian constitution, which allowed any citizen of good standing to leave the country. After one warning, he was arrested and thrown in jail without trial..."
Waungwana, jisomeeni mwenyewe hapa. Uongo bin nuksi!
Ni nini maoni yako? Kama mtanzania, nini tunaweza kufanya kujikinga na watu kama hawa? By the way huyu jamaa ni mtanzania kweli?
Mawazo yangu ya nini wee na mimi tunaweza kufanya kukomesha hii nuksi = next posting.
Ned

11 comments:

Anonymous said...

Tumeshakaribia kijiweni. Karibu sana.

John Mwaipopo said...

Tumeshakaribia sasa tunasubiri kahawa tu.

Anonymous said...

Hii habari ya huyu jamaa mbona haikuwahi kutokea kwenye vyombo vya habari Tanzania? Au wengine tulipitwa na kisa hiki? Je hizo visa alitoa kwa wapinzani gani wa serikali hadi akatiwa matatani?

ned said...

Wazee, nipo
Awali... bwana Ndesanjo, hivi kuna namna ambayo naweza ku-mwongeza mtu kwenye members' list simply kwa kubonyeza comment zake? Nina struggle kuongeza mtu mmoja mmoja... na inakua kazi kidogo:)
By the way - Ndesanjo na mwakyagi sikuweza kupata email zenu ili kuwaruhusu ku-post stories - ndio maana ya kijiwe Kila mtu anaweza kuja na story safi.

ned said...

By the way,
huyo jamaa wa Seattle ni fix ile mbaya... nitatuma nakala ya email ambayo nilikuwa nimehamasisha baadhi ya wabongo hapa - tumlipue. Ingawa kuna madongo yameshaanza kutupwa )kuna watu wanaona kumlipua huyu jamaa ni noma... eti ni mtu anatafuta riziki yake...
Kwa maoni yangu, jamii tunaitengenza wenyewe.. iwapo ni OK kwa mtu kuharibu jina la kamii nzima ili tu kapata kitu kwa ajili yake binafsi... ni nini mwisho wake?
Ned

mzee wa mshitu said...

Nimekaribia kijiweni mbona sioni benchi au tutakaa katika nyasi tuendelea kusogoa, safi sana mshkaji!

Jeff Msangi said...

Nimekaribia kijiweni.
Hii porojo ya huyu "Emil" inatia kinyaa kabisa.Nilipoona tu palipoandikwa "when a new political party took power" nikajua mushkeli.Tanzania chama tawala kimebakia CCM..Nadhani wamekosea nchi hawa.Kuna umuhimu wa kuwarekebisha watu kama hawa.Tafuta riziki yako kwa heshima na wala sio upuuzi wa namna hii.

Jeff Msangi said...

Jamani,
Mimi mambo ya namna hii huwa yananiudhi sana.Kujidhalilisha mara nyingi tunataka wenyewe.Nimechukua hatua ya ziada,nimewapigia simu hao jamaa na kuwaomba wachunguze zaidi vitu kama hivi kabla ya kuviandika na kuvichapisha.

ned said...

GOod for you Jeff,
kuna jamaa kadhaa ambao nafahamu wamejaribu kufuatilia. Nilimwandikia mhariri kutaka afanye uchunguzi na kama ikigundulika kuwa story ni fake... a run another story kukana yaliyoandikwa awali. Alijaribu kujitetea kuwa si yeye aliyeandika hiyo story... lakini akasema atafuatilia.
inabidi tuendelee kutia shinikizo.
nadhani Jeff unaweza kuwa sahihi... hasa kuhusu kuchanganya majina ya nchi. Lakini maadamu jina Tz lipo kwenye hiyo article, inabidi tuendelee kufuatilia

Anonymous said...

Kwa ufupi naona hakuna haja ya kumharibia maisha huyu jamaa. Watu wengi wanajaribu kila waliwezalo kuja katika nchi hii ya asali na maziwa. Kwa vyovyote hali ngumu ya maisha ndo imemfanya labda kufikia kiwango hicho. Na vilevile kama kweli amedanganya, basi anastahili pongezi. Halafu si vema kuingilia biashara za watu. Tukianza mtindo huo ugenini, ina maana zile tabia za kiswahili bado zinatuandama hadi huku. Hiyo ni dalili ya wivu. Huku kila mtu ana-mind business zake. Kumbukeni kwamba vile vile mambo ya dini ni biashara kama vile siasa. Kama uongo wake umemsaidia kupata riziki na kuwasaidia ndugu zake aliowaacha nyumbani, hilo ndo la muhimu.

Anonymous said...

ndio tatizo letu sisi wabongo. hatupenda kurekebisha wenzetu. ndio mana matatizo yetu nyumbani hatuwezi kurekebusha na kuendelea. kwa mfano, jamaa anaiba ofisini, anashikuwa na anaachishwa kazi. tutatkuwa wakwanza kumshambulia, lakini akiomba character reference, tunampamba kama vile alikuwa mtu mzuri kweli. ndio unakuta watu wanaendesha rushwa na kuiba kwenye mashirika. how then do u turn around and say corruption should be stopped. ni sisi who are morally corrupt.