Monday, May 28, 2012
Jumamosi tarhe 26 May, "Ka"-kikundi kinachojiita "Jumuia ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam" kiliamua kuingia mitaani kufanya maandamano (hiyo juzi na pia jana asubuhi) ya kushinikiza kura ya maoni kabla ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.
Katika kufanya hivyo waandamanaji hao waliishia kuchoma makanisa na magari na kuharibu mali za watu! Kwa ufupi waliishia kuvunja amani na utulivu. Kikundi hiki kinajulikana kama kinadai muungano kati ya Zanzibar na Tanzania bara uvunjwe ili wao "waachiwe Zanzibar yao" na wawe huru kuifanya kuwa nchi ya kiislam yenye kuongoza katika misingi na sheria za dini hiyo. Potelea mbali wazanzibar wenye dini nyingine - hilo wao hawaoni kama issue!
SIPINGI kabisa uhalali wa watu kutoa maoni yao, na wala sipingi uhalali wa watu kufuata taratibu tulizojiwekea na kufanya maandamano ya amani ili kuweka wazi mawazo, maoni au hata malalamko yao! Heck hata sipingi kwa wazanzibar kutaka kuvunja muungano... kama hayo ni maoni ya wazanzibar walio wengi - what can we wa Tanzania bara do to stop them? - nothing!
Lakini pamoja na kuyasema hayo; Sina budi kulaani kwa nguvu zote kilichotokea Zanzibar over the weekend! Ukweli ni kwamba tabia hii ya kuingia mitaani na kuanza kuharibu nyumba za ibada nam ali za raia wasio na hatia - ni tabia ya kihuni na yenye kudhihirisha kufilisika kimawazo na kuishiwa nguvu ya hoja. HATA siku moja matumizi ya nguvu na uvurugaji wa amani hauwezi; na wala hautakaa ulete mabadiliko ya kweli! Wengi wa wanao support matumizi ya nguvu wanaweza kubisha - na hata kuhalalisha matumizi ya vurugu kama njia mbadala iwapo "njia zote nyingine zimekwama". Kwa bahati mbaya, sijaweza kukutana (and I am very open kuingia kwenye majadiliano na mtu kama huyo) - sijaona yeyote ambaye ameweza kunifahamisha kuwa njia ambazo zimeshatumika ni a, b, c, d na zimeshindikana! Ndugu zetu hawa, hawana hoja yenye nguvu, hawana uwezo wa kujenga hoja, hawana uwezo wa kuwakilisha mawazo yao na kuelimisha jamii kile wanachokisimamia, na wala hawana uwezo wa kutetea kile wanachosimamia! Wanachofanya ni kuwajaza watu chuki, kwa sababu ambazo hazina mshiko - na wao wanajua wazi kabisa kuwa hoja zao hazina mshiko - si wa kielimu, si wakijamii si wakisiasa, na si wakidini - mshiko "mayolo"/ none / zuch!!! wanalijua hilo; lakini bado tu wanang'ang'ania kuendelea kuanzisha na kuchochea vurugu.
Hata kama nia yao ni kufanyika kwa hiyo kura ya maoni, wanajua kuna njia na taratibu ambazo zipo wazi! Na iwapo mtu huridhiki na taratibu hizo kuna ruksa na njia za kuzi-challenge. Ajabu sana kusikia mtu anadai kura ya maoni kwa nguvu... Mbona zoezi kama hilo si geni Zanzibar?
Thankfully the Field Force Unit - FFU were released to roam the streets, waandamanajo 30 kukamatwa and the rest run to their homes☺. Wakati amani inaonekana kurejea katika mitaa ya "mji mkongwe" Zanzibar, ukweli nashindwa kujizuia ku ainisha my wish... Natamani sana kama serikali ya mapinduzi inge waashushia hawa jamaa (na wote wenye hii akili za kipuuzi kama hizi hile peace seems to have been restored, I just wish they find whoever is behind this stupid stunt and make a lesson out of them.
Nakutakia siku njema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
I visited several web pages however the audio quality
for audio songs existing at this website is truly fabulous.
Post a Comment