Thursday, September 04, 2014

UNAFIKI MBAYA SANA!

Ukweli unafiki kitu mbaya! Hivi inakuwa je mtu akikuunga mkono; kwako ni shujaa na unamuimbia sifa kibao! Mtu huyo huyo kesho akionyesha kuwa na msimamo ambao wewe huukubali, mara anakua adui, na unaanza kummwagia matusi kibao!
Kupo wapi uwezo wetu wa kuheshimu mawazo na uhuru wa mtu kuji-express? Kupo wapi uhuru wa kuchangia na kuweka hadharani mawazo yako, bila kuwa na hofu ya kupigwa mawe, kutukanwa na kubezwa?
TUnajenga nchi ya watu wa namna gani iwapo kila mwenye wazo au msimamo tofauti na wako ni adui?
watanzania ni LAZIMA tuamke, tuheshimu mawazo ya watu WOTE ikiwa ni pamoja na mawazo yanayokinzana na misimamo yetu!
Kubadilika na kuanza kumpiga mtu mawe na matusi - simply kwa kuwa ana mawazo tofauti na yako - HUO NI UNAFIKI wa kiwango cha juu kabisa! TUBADILIKE!